Habari za wakati huu wapenzi wa hadithi fupifupi na ndefundefu. Naam, nakukaribisheni kwa mara nyingine tena kwenye makala yetu hii ya 'MJUE MUANDISHI NA KALAMU YAKE' ninae kuletea makala hii ni mimi Zubery Razuur Mavugo. Leo tuta yatazamia maisha ya Muandishi kwa jina la Frank Masai.
HISTORIA YA MAISHA YAKE KWA UFUPI.
Kwa majina anaitwa Frank Masai[hatuja fanikiwa kujua zaidi maana ya majina yake kwakuwa makala yetu ni bado ni mbegu]. Amezaliwa tarehe
27 mwezi wa 6 mwaka 1988 huko Bukoba. Kabira lake ni mfipa, mtu wa Sumbawanga, dini yake ni mkristo. Amesoma, elimu ya awali, msingi, kidato hadi chuo.
NDOTO ZA KUWA MTUNZI WA MAANDISHI.
Ndoto za uandishi zimeishi akilini mwa kijana huyu toka zamani. Kwa mara ya kwanza Frank Masai alishawishika na kuishikilia kalamu rasmi alipokuwa kidato cha pili, na aliandika baada ya kuvunjika kwa penzi lake kipindi hicho.
''Mara ya kwanza kushawishika kuandika hadithi nilikuwa kidato cha pili (2005) nilipokuwa katika mahusiano yangu ya kwanza kabisa. Yalipovunjika ndipo nikaamua kuandika hadithi fupi tu ambayo sikuandika kwa umakini kabisa lakini ilihusiana na mahusiano yangu yaliyovunjika. Hadithi hiyo niliiandika kwenye makaratasi ya kujibia mitihani ya taifa. Makaratasi yale yalikuwa kama jarida hivi, kwa hiyo nikaandika humo.'' Frank Masai alisema maneno hayo siku moja alipohojiwa na mmoja kati ya waandishi wa kurasa ya Habari za Waandishi.
Frank Masai kwanzia hapo ndipo alipobaini kumbe licha ya kuwa mwanafunzi, vilevile mwenyezi Mungu amemjaalia kipaji cha kuandika, mapenzi yakawa yamemfanya atambue kipaji chake ingawa hakuwa na imani nacho sana.
KUJIINGIZA MTANDAONI.
Frank Masai, alipomaliza elimu yake ya chuo mwaka 2012, alikuwa mpweke sana, kwani alijizoesha muda mwingi kusoma lakini kwa wakati huo hakuwa akisoma kitendo kilichomfanya asiwe na furaha.
Kukuwa kwa kasi kwa mitandao ya kijamii, kulimfanya Frank Masai nae atamani kujiingiza humo ilinae akashuhudie nini kilichowasukuma watu wawe ndani ya mitandao hiyo.
Mwaka 2012 huohuo, Frank Masai akajiingiza rasmi ndani ya mitandao ya kijamii hasa mtandao wa Facebook. Alijiingiza kama mwana jamii yeyote mwenye kuhitaji kujifunza mambo mbalimbali yanayohusu jamii, pamoja na kuchati na watu mbalimbali, lakini hakuwa na mawazo ya kuandika ndani ya mtandao huo.
Akiwa mtandaoni, alifanikiwa kulike page mbalimbali za waandishi, ndipo akakutana na page moja iliyojulikana kwa jina la ''UWANJA WA SIMULIZI'' kipindi hicho George Iron Msonya [Muandishi] nd'o alikuwa akirusha hadithi zake ndani ya uwanja huo. Ingawa ni miaka minne sasa tangu aanze kusoma hadithi mtandaoni na ni hadithi za watu wengi sana alipata fursa ya kuzipitia, lakini hata kidogo, hakuwasahau waandishi aliyowakuta wakiandika hadithi kwa kushirikiana na George Iron Mosonya.
''Mara ya kwanza kuingia mtandaoni ilikuwa ni 2012 nilipomaliza chuo. Nilikuwa naboreka sana kukaa peke yangu bila kazi, ndipo nikaingia mtandaoni (facebook) na kukutana na ukurasa na kundi la UWANJA WA SIMULIZI kipindi hicho George Iron alikuwa ndio mtu anayeweka kazi zake huko. Na Frank Mushi pia nakumbuka bila kumsahau Nyemo Chilongani.'' Frank Masai alisema.
Aliongeza kwa kusema kuwa, ''nilikuwa msomaji tu! Sikuwahi kufikiria na mimi kuandika, ila niliposoma 'TAALUMA ILIYOPOTEA' kwa mara ya kwanza 2013, ikanifanya niandike mwenyewe bila kupenda. Nilinunua hadi kitabu chake aisee. Ilikuwa imeshiba ile kazi. Naweza sema ndio ilinifanya niandike mtandaoni ile kazi huku nikipata ushawishi wa kuendelea kuandika toka kwa Iron Mosenya''.
Hadithi yake ya kwanza kabisa mtandaoni, ilikuwa ni 'Mawio na Machweo' ila kutokana na sababu zake binafsi aliamua kuikata na kuandika nyingine aliyoiita 'Ukijua Utakufa' hadithi hiyo, yenyewe hakuikata bali aliiandika yote hadi mwisho na baadae ndipo alipoiandika hadithi ya 'MY ROSE' ambayo ndio ile aliyoiandika kiufupi pindi alipokuwa kidato cha pili, lakini safari hii aliiandika kwa marefu na mapana zaidi hadi alipoimaliza, kisha akaimalizia ile hadithi yake ya 'Mawio na Machweo'.
CHANGAMOTO.
''Changamoto nyingi zilikuwa ni kutoka kwa wadau na mashabiki. Nilikuwa mdau pia na shabiki, bado akili yangu ilisimama vilevile kama shabiki na mdau, sikujua kuwa tayari nilikuwa kioo cha jamii. Hivyo hilo tayari lilikuwa tatizo kwani niliweza hata kutukana na kutukanana na mashabiki wengine.
Changamoto hiyo ilifikia kupoteza baadhi ya wadau na marafiki ambao tayari niliwaunda. Nakumbuka niliwahi rushiana matusi na mdau mmoja hivi, daaaah! Hiyo kwangu nasema ndio kipindi kichafu sana nilichokipitia. Na tangu hapo, ikabidi nijitambue.
Changamoto nyingine ni kukatishwa tamaa tu, kuambiwa huwezi mara hujui, mara kihadithi chako kifupi kama kimini. hahaaa [Alicheka kiaina]. Lakini nimshukuru kwa mara nyingine George Iron, alikuwa akinipa moyo na leo nipo hapa.'' Masai alieleza hayo.
MAFANIKIO.
''Mafanikio niliyoyapata, siwezi sema ni madogo, ni makubwa sana. Ukitaja waandishi bora kumi wa riwaya fulani leo hii, ni dhambi kama utaliacha jina la Frank Masai. Najitahidi kwa uwezo wangu niliojaaliwa na Mola, na nashukuru napokelewa vema. Hayo ni mafanikio pia, jina langu hata nikifa leo, bado litaishi.'' Alisema.
SHUKRANI.
''Wadau na Washabiki wangu, mimi sina cha kuwalipa kwa mioyo yenu na sala zenu za kheri kwangu. MUNGU ni muweza wa yote na leo hii nipo hapa nilipofika kwa sababu ya uwepo wenu. Sina cha kuwalipa zaidi ya kuwaambia kuwa nawapenda sana na mtegemee mazuri kutoka kwangu. Asanteni sana.'' Masai aliweka kituo hapo.
**********************
MTUNGAJI WA MAANDISHI HUYU ANAPATIKANA KWENYE PAGE YAKE IJULIKANAYO KWA JINA LA ''NYUMBA YA TUNGO NA SIMULIZI'' UKIWA KAMA MDAU WA HADITHI UNAOMBWA UFIKE HUKO ILIKUSHUHUDIA NI JINSI GANI MTUNZI HUYU ALIVYOBALIKIWA KALAMU YENYE KUONA MBALI.
AHSANTE, TUKUTANE TENA JUMAMOSI IJAYO KWA AJILI YA KUWAJUA WATUNZI WETU.
IKUMBUKWE KILA JUMA MOSI NA JUMA TANO TUTAKUWA TUKIPATA FURSA YA KUWATAMBUA WATUNZI WETU PAMOJA NA KALAMU ZAO HAPAHAPA KWENYE UKURASA WA HABARI ZA WAANDISHI. AHSANTENI.
KWA SABABU NAKUPENDA Nitakuwa nawe Daima |