12 Jan 2016

MKONO WA MWANDISHI..Na. Hassan Mambosasa

MKONO WA MWANDISHI..Na. Hassan Mambosasa










MAKALA
MKONO WA MWANDISHI...
Bado tunaendelea katika msimu wetu huu wa tatu wa kutazama kazi mbalimbali za waandishi, baada ya kuutazama mkono wa Molito wiki iliyopita leo hii kalamu yangu imemwangukia HASSAN MAMBOSASA au wengi mnamtambua vyema kwa mikasa yake ya kuvutia inamhusisha mpelelezi maarufu wa serikali Norbert Kaila, mzee wa totoz.

Makala hii moja kwa moja inatua hukoooooooo Songea katika chuo cha St Joseph ambapo kijana huyu mtundu wa fasihi ndiko alikojificha kwa miaka hii akiongeza taaluma nyingine ya TEHAMA. Ni kijana mpole, mwembamba, kaenda hewani sekunde, ukimtazama harakaharaka huwezi kumzania kama huyu ndiye Hassan Mambosasa ambaye mkono wake huwa hutuletea burudani zinazotuacha na taharuki ya hali ya juu.
Ka mpenzi wa kurasa ya Riwaya Maridhawa ndani ya mtandao wa kijamii wa Facebook atakuwa amekwishauona mkono huu katika kazi zake kama
SADAKA
MALI HARAMU
KUWADI
NORBET KAILA
MWANGAMIZI
JINAMIZI
KOSA
DHAHAMA
WAKALA WA GIZA
SHUJAA
NSUNGI
WITO WA KUZIMU
Hizi ni kazi ambazo mkono huu adimu umeziandika kutoka kwenye fikra pevu zinzzojua nini cha kuwapa wana wa Adam. Nilipomuuliza kama kazi hzi zote keishaziweka kwa washabiki akanambia hapana, kazi ambazo washabiki wameziona ni tano tu kati ya hizi, na hizo ambazo hazijasomwa anasema ni moto wa kuotea mbali kwani mkono wake umefanya kazi katika teknolojia ya 3D.
Norbet Kaila mzee wa totoz ndiye anayeutambulisha rasmi mkono huu, kwani visa vyake vimekuwa vikitamba sana kwenye kurasa ya Riwaya Maridhawa na sas kwenye Jamvi la Simuliza za Kusisimua ambako riwaya ya Wakala wa Giza imeshika kasi ya ajabu.
Mkono huu wa Hassan Mambosasa umefanya kazi nzuri sana kwenye riwaya ya SADAKA ambayo labda haujawahi kuisoma. Riwaya hii ambayo yeye mwenyewe anasema kuwa ni riwaya ambayo hawezi kuisahau na haitamtoka kichwani mwake na kama ukimwambia akwambie ni kazi ipi kwake ni bora sana kuliko zote yeye angekwambia ni SADAKA. Kuna nini dani ya kazi hii hebu tuangalie kwa kifupi.
>>>>>>>>>>>>>>SADAKA<<<<<<<<<<
NDANI ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam kijana wa mwaka wa kwanza aitwae Johnson Lumaki anatokea kuvutiwa na msichana aliyekuwa mwaka wa kwanza anayeitwa Janeth Thobias Londo, jitihada zake za kujaribu kufikisha ujumbe kwa mlengwa zinamuwia ngumu sana kutokana na hali duni aliyokuwa nayo. Matusi na kejeli ndicho kitu kilichokuwa kinamkumba kila wakati lakini hakuchoka kabisa hadi ikafika anatukaniwa baba yake aliyefariki. Kijana huyu akapatwa na shinikizo ghafla kisa kumpenda huyo binti wa kitajiri.
Upande mwingine kikundi cha watu waliokuwa na utumishi wa shetani walikuwa wakitafuta kila njia waweze kutawala dunia, vijana saba wenye nguvu za ajabu (superhero) kutoka mataifa tofauti walihitajika kutolewa sadaka kwa kuchinjwa ndivyo wafanikiwe. Vijana watano kama hao walikuwa wameshatolewa sadaka na walikuwa wamebaki wawili tu waliokuwa barani Afrika. Thobias Londo babamzazi wa Janeth akiwa kiongozi wa jamii hiyo nchini anapewa alama za kijana huyo mmoja maybe alihitajika kutolewa sadaka.
Siku kadhaa mbeleni Janeth anapania kumkomesha Johnson kwa kumwambia kuwa alitaka kwenda naye Kilwa Kisiwani kutembea na kutalii, huko alikuwa na lengo aende na vijana ambao wangempiga hadi kumuumiza vibaya. Maajabu ya Johnson yanaanza kuonekana hapo kwa kupigana na vija hao mpaka kuwashinda kwa umfundi wa hali ya juu, alipotaka kumfuata Janeth amtie adabu walivamiwa na kundi la majambazi ambao walitaka kumteka Janeth. Anamuokoa Janeth na kuwa karibu na Mzee Londo aliyepewa kazi ile maalumu na jamii yake ……
>>>>>>>>>>>>>>>>>
Ndugu msomaji huo ni muhtasari tu wa kazi mojawapo ya mkono wa Mambosasa.
Kumbuka hii ni makala yako maridhawa kabisa ya Mono wa Mwandishi na leo hii huyu hapa Hassan Mambosasa. Ukitaka kupata riwaya zilizojawa na ufundi wa fasihi basi mkono huu ndiyo hasa utakuonesha umahiri wa sanaa hiyo. Mkono huu amabo sasa unaandika zaidi upelelezi chini ya Norbet Kaila N001, bila shaka mwenyewe utasema ‘ndiyo’ kwa kazi zake kali kama KOSA ambayo imeandikwa kwa ufundi wa hali ya juu sana au WAKALA WA GIZA inayozungumzi kisa ambacho kitakuacha kinywa wazi mpaka unamaliza kazi hiyo. Ukianza kusoma riwaya yoyote iliyoandikwa kwa mkono huu hakika hautatamani kula wala kulala na hautatamani iishe bali ungetamani uendelee kuisoma kwa jinsi ambavyo mkono huu unavyoihuisha fasihi ndani ya kichwa chako na kuugeuza ubongo wako kuwa uwanja wa mapambano makali.
Mwenyewe anakili wazi kuwa katika mtandao wa facebook kazi ya WAKALA WA GIZA ndiyo haswa ilipokelewa vyema na washabiki.
Lakini nilimwuliza kwa nini anapenda sana kuandika kazi za kipelelezi naye alinijibu hivi ..
“Ni kitu ambacho ni kigumu kukielezea sana sababu maalum ila napenda niseme nimeona ni njia muafaka ya kufikisha ujumbe kwa jamii ambao unahitaji kuwa bayana zaidi”.
Kutokana na umahiri wa kuandika kazi hizi za Kipelelezi Mambosasa anaondokea kuwa mkali wa aina hii ya simulizi ukiachilia mbali wale wakongwe ambao kamwe hatuwezi kuwagusa lakini kwa kizazi cha sasa anakuja kasi na we mwenyewe ni shahidi.
Mkono wa Mambosasa unakuahidi kukupa vitu vikali sana mwaka huu ambavyo vitakufanya uone vipaji adimu vilivyojificha hapa Tanzania.
Nisikuchoshe wala usinichoshe fuata link hii hapa ukaone mwenyewe kazi za mkono huu…
Naomba nikuache na nikutakie jumamosi njema tuonane tena wiki ijayo hapahapa ni mkono wa nani tutauangazia, kodoa macho!
0766974865







Translate