MKONO WA MWANDISHI
Kwanza kabisa napenda kukutakia heri ya mwaka mpya, wapo wengi ambao wangependa kuuona mwaka huu lakini mapenzi ya Mungu hayakutaka iwe hivyo kwani ajali za barabarani, magonjwa na mambo mbalimbali yamechukua maisha yao.
Je mimi na wewe ni nani hata tusimshukuru Mungu kwa hili?
Je mimi na wewe ni nani hata tusimshukuru Mungu kwa hili?
Naanza kwa kuwatakia heri na Baraka kwa mwaka huu mpya wa 2016 naamini kila mmoja keishajipangia mambo ya kufanya mwaka huu, na huo ndiyo mtindo wa maisha unaowafanya watu kufika pale wanapotaka.
Katika program yetu hii ya Mkono wa Mwandishi inayokujia hapa katika kurasa ya Habari za Waandishi, inafungua mwaka kwa kutazama mkono wa Hussein O. Molito. Jina hili si geni kwa wapenzi wa riwaya katika mitandao ya kijamii, nikilitaja tu basi tayari umeshajua ni nani namzungumzia katika tasnia hii ya uwandishi wa riwaya.
Hussein O. Molito anayemiliki kurasa ya Tungo Za Hussein O. Molito…. Sasa hivi ameuanza mwaka na stori yake ya Moyo Mpweke ni mwandishi mbunifu mwenye mvuto wa aina yake kwa washabiki. Hali hii imempelekea kuwa na mafanikio makubwa na kuongeza mtazamao katika kazi yake kwa ujumla akiwa na ndoto za kupanua wigo wa sanaa yake.
Kwa wale washabiki wa mkono huu wanautambua pindi tu wakisikia jina hilo akilia yao hugonga vichwa na kukumbuka mikasa kama
* THE STRANGER
* LOVE BITE
* ALICE THE SUPER STAR
* MCHORO WA AJABU
* THE GIRLS IN ISLAND
* JINI KIPEPEO
* THE JUNKLE
* MACHOZI YA PLASTIKI
* MAPIGO YA MOYO
* ALL OF ME
* SHE IS NOT ALIVE
* LOVE BITE
* ALICE THE SUPER STAR
* MCHORO WA AJABU
* THE GIRLS IN ISLAND
* JINI KIPEPEO
* THE JUNKLE
* MACHOZI YA PLASTIKI
* MAPIGO YA MOYO
* ALL OF ME
* SHE IS NOT ALIVE
Na nyingine nyingi zilizo na zinazotamba katika Facebook na Whatsapp. Mkono wa kijana huyu hakika unafanya kazi nzuri, makini na inayosisimua na inayokubalika na washabiki wengi wa riwaya, katika riwaya yake ya Mapigo ya Moyo, Molito anasema… nanukuu…
“Moyo ni kiungo kidogo sana katika mwili wa binadamu. Lakini ni muhimu kuliko mwili wenyewe. Mtu huumia zaidi akiumizwa moyo kuliko mkono. Maumivu ya mkono madaktari huweza kuyabadili kwa njia mbalimbali ikiwemo sindano za ganzi. Lakini maumivu ya moyo yanaweza kukaa milele na kukufanya ukose raha ya maisha yenyewe…”
Maneno haya yanaubeba umahiri wa mkono wa mwandishi huyu ambaye sasa ana ndoto kubwa ya kuwekeza katika filam za Kiswahili. Wengi wanajiuliza kwa nini Molito hupenda kuandika hadithi zinazohusisha majini? Yeye mwenyewe anajibu hapa chini…
“…Mara ya kwanza kwenye utambulisho wangu Facebook watu walinipokea vizuri kwenye riwaya ya Stranger, hivyo kila niandikapo riwaya za viumbe ambao si binaadamu… mashabiki husisimka na kupata wafuasi wengi. Hata kwenye mauzo riwaya za kijini zinalipa zaidi kwangu…”
Hii ndiyo siri yake ambayo leo ameamua kutuwekea hadharani na watu wote tumeijua. Hakika labda wapo watu waliojua kuwa Molito ana mahusiano ya karibu na viumbe hawa lakini sivyo bali ubunifu wa mkono wake unaocheza na karamu huwa unajua kung’amua shabiki anataka nini na ndiyo maana akaja na staili hii ya aina yake ambayo hakuna mwandishi anyeweza kuiiga kwa sasa labda wale wa zamani zileeee za Alfu Lela Ulela.
Mkono huu umeandika riwaya nyingi nzuri ambazo wewe mwenyewe ni shahidi kwa jicho lako limesoma, akili yako ikaburudika na mwili wako ukasisimka hata kuufanya usiku wako kuwa mgumu. Hii ndiyo fasihi, msanii wa maandishi anapocheza kwa ufasaha na maandishi yake basi hapo huifanya fasihi kuishi, fasihi kuwa hai.
Pamoja na kazi zote hizo Molito anasema hatoisaha ‘Alice The Super Star’ ambayo kwake imekuwa riwaya bingwa kati ya nyingine zote. Anasema riwaya hii katika mauzo imemwingizia zaidi ya Shilingi za Kitanzania Milioni 2, na riwaya hii kiukweli ilipokelewa vyema na watu ilipotoka hadharani.
Kwa wale ambao hajapata kuzipitia kazi za mwandishi huu na kuona mkono wake unafanya nini katika fasihi, hii hapa ni synopsis ya riwaya ya Alice The Supestar ….
Molito anaielezea kwa kifupi…
“…Ni riwaya iliyojikita kwenye maisha halisi. Inahusu shabiki mmoja aliyetokea kumpenda super star huku kipato chake kikiwa kidogo kiasi cha kushindwa kulipia hata kiingilio tu cha kuangalia show hadi kufikia kutimia ndoto zake za kumuoa.
Ndani kuna majonzi, furaha, chuki, visasi, usaliti, ubaguzi, mauaji, upelelezi, rushwa na visanga kibao. Kwa ujumla nimegusa kila kitu kitendekacho kwenye jamii iliyotuzunguka.”
Hebu tuone kidogo utamu wa kazi hii ya ‘ALICE THE SUPER STAR’
††††††††††
Sauti ya mwanadada aliyebarikiwa kila aina ya vipaji ambavyo kwa pamoja anavitendea haki vipaji vyake, ndio iliyonifanya mimi nitamani kumsikiliza kila niisikiapo sauti yake.
Si mimi tu niliyeiona thamani ya sauti ya mwana dada huyo, ila kila mvulana alisikiapo jina la ALICE, basi moyo wake ulikiri uzuri wa kila kitu alichojaaliwa mrembo huyo.
Napenda anavyotangaza, napenda anavyoimba, napenda anavyoigiza pia napenda kumtazama kila nimuonapo kwenye mabango ya matangazo mbali mbali ambayo makampuni mengi yalikua yana mtumia mrembo huyo kwenye kuvutia biashara zao.

Ilifikia kipindi mpaka kampuni inayotengeneza sabuni, waliamua kutumia jina lake na picha yake kwenye sabuni hiyo iliyo pewa jina la Alice.
Hapo waliweza kunipata kwa kuitumia sabuni hiyo tu, si kwa sababu ni nzuri kuliko sabuni zote, ila Alice alikua ni mzuri kuliko kitu chochote katika mboni za macho yangu.
Geto langu limejaa picha zake nilizokata kwenye magazeti mbali mbali, hadi kufikia wakati nilitamani kwenda kwenye tamasha lolote ambalo nitasikia Alice ata perform japokua kipato changu kidogo.
Sikuweza kuamini macho yangu siku nilipokutana na Alice macho kwa macho huku tabasamu zito lililojaa bashasha likiwa linanilenga mimi. Niliishiwa nguvu hadi kauli baada ya kuona superstar huyo akiwa mbele yangu na kunitazama kwa macho yake malegevu.
Kwa mara ya kwanza nilipata nafasi ya kugusanisha mikono yangu na mikono yake.

“nimesikia wewe ni fundi mzuri… nimekutafuta sana LARRY ……naomba unisaidie.”
Nilipigwa na butwaa baada ya kugundua kua alikua ananitafuta mimi kwa muda wote, pia niliamini kua lile tabasamu lilikua la furaha ya kuniona baada ya kunitafuta kwa muda mrefu.
Hii ni nafasi yangu pekee ya kuonyesha hisia zangu kwa mrembo huyo… je nitafanikiwa?... atanidharau kwa sababu mimi kapuku?.... au atanikubali ili nitimize ndoto zangu zilizokua zimekufa muda mrefu?

††††††††††††
Hayo na mengine mengi.. utayapata kwenye riwaya hii ya kusisimua.
Mwisho kabisa hili ni neno la Hussein Molito kwako shabiki wa kweli…
“Mwaka huu ni mwaka wa kujiandaa kwa vitu vingi vikubwa. Kwanza kutakuwa na website kabisa ya kazi za Molito. Kutakuwa na Movie kabisa bila kusahau vitabu katika mfumo wa hard copy”.
Hussein Molito anawaambia … “Wategemee mengi kutoka kwangu… coz nina riwaya ya kipelelezi ambayo kwangu mimi naiita mapinduzi ya waandishi wote waliojibebea majina kwenye riwaya…
Ili kusoma kazi nyingine nyingi za mtunzi huyu na kuujua vyema mkono wake bofya link hii hapa chini...
Niwatakieni mwaka mpya mwema sana kwenu nyote.
Toa comment yako ili tujue nini tuboreshe kwenye makala hii, au tuuangazie mkono wa nani.
Toa comment yako ili tujue nini tuboreshe kwenye makala hii, au tuuangazie mkono wa nani.
Adios amigos…
0766974865.
0766974865.